لِلۡفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحۡصِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ ضَرۡبٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ يَحۡسَبُهُمُ ٱلۡجَاهِلُ أَغۡنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعۡرِفُهُم بِسِيمَٰهُمۡ لَا يَسۡـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلۡحَافٗاۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ ٢٧٣
Lil-fuqarā'il-ladhīna uhsirū fī sabīlillāhi lā yastatī'ūna darban fil-ardi yahsabuhumul-jāhilu aghniyā'a minat-ta'affufi ta'rifuhum bisīmāhum lā yas'alūnan-nāsa ilhāfan wamā tunfiqū min khayrin fa innallāha bihī 'alīm
Nawapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiye wajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Na kheri yoyote mnayo toa, basi kwa yakini Mwenyezi Mungu anaijua. 273
Maelezo ya chini
273 Na kutoa huko ni kwa kuwapa mafakiri ambao kwa sababu ya kuwania jihadi hawawezi kujichumia wenyewe, au ambao kwa sababu ya kuumia katika jihadi wameemewa na kuweza kuhangaika katika nchi kutafuta riziki. Na juu ya hivyo wanajizuia na kuomba omba. Asiye wajua huwadhania kuwa ni matajiri, lakini wewe utajua hali yao kwa alama zake. Na kila mtacho kitoa kwa wema, basi Mwenyezi Mungu anakijua, naye atakulipeni malipo ya kutosha.