Surat Al-Baqarah, aya 272

2:272

۞ لَّيۡسَ عَلَيۡكَ هُدَىٰهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَلِأَنفُسِكُمۡۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ ٱللَّهِۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يُوَفَّ إِلَيۡكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تُظۡلَمُونَ ٢٧٢

Llaysa 'alayka hudāhum walākinnallāha yahdī man yashā'u wamā tunfiqū min khayrin fali'anfusikum wamā tunfiqūna illabtighā'a wajhillāhi wamā tunfiqū min khayrin yuwaffa ilaykum wa antum lā tuzlamūn

Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na kheri yoyote mnayo toa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mtakayo toa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa. 272

Maelezo ya chini

272 Si juu yako wewe, ewe Muhammad, kuwaongoa hao walio potea au kuwalazimisha watende kheri. Lilio juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na msaada wowote mnao toa kumpa mtu, faida yake inarejea kwenu wenyewe. Mwenyezi Mungu atakulipeni kwayo. Haya ni hivyo ikiwa mnapo toa hamkusudii ila kumridhi Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mnayo itoa kwa njia hii itarejea kwenu, na mtazipata thawabu zake kwa ukamilifu bila ya kudhulumiwa chochote.