Surat Al-Baqarah, aya 174

2:174

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡتُمُونَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَشۡتَرُونَ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَٰٓئِكَ مَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ إِلَّا ٱلنَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ ١٧٤

Innal-ladhīna yaktumūna mā anzalallāhu minal-kitābi wayashtarūna bihī thamanan qalīlan ulā'ika mā ya'kulūna fī butūnihim illan-nāra walā yukallimuhumullāhu yawmal-qiyāmati walā yuzakkīhim walahum 'adhābun alīm

Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa moto, wala Mwenyezi Mungu hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao watapata adhabu chungu. 174

Maelezo ya chini

174 Miongoni mwa watu wanao jua aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu kipo kikundi kinacho ficha baadhi ya maandishi ya ufunuo kwa ajili ya sababu fulani za kilimwengu. Mayahudi, mathalan, wakificha mengi yaliyo kuja katika Taurati ya kueleza sifa za Mtume kwa kukhofu wasije wakasilimu watu wa mila yao na kwa hivyo utukufu wao ukaondoka na wakapoteza mapato yao na vyakula vyao vitamu. Na hakika chakula chao wakilacho kwa njia hii ni kama kula moto, kwani hayo yatawapelekea kuingia Motoni. Mwenyezi Mungu atawatupilia mbali Siku ya Kiyama, wala hatawasafisha uchafu wao, na mbele yao kuna adhabu ya kuumiza kweli.