حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٠٥
Haqīqun 'alā al lā aqūla 'alallāhi illal-haqqa qad ji'tukum bibayyinatim mir rabbikum fa arsil ma'iya banī isrā'īl
Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami. 105
Maelezo ya chini
105 Na mimi pupa yangu ni kumsemea kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na nimekujieni na Ishara yenye shani kubwa, yenye hoja iliyo dhaahiri katika kubainisha Haki niliyo kuja nayo. Basi waachilie waje nami Wana wa Israili, na uwatoe kwenye utumwa wa kahari yako, wende nami kwenye nchi nyengine isiyo kuwa yako, na huko wapate kumuabudu Mola Mlezi wao na wako.