وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٠٤
Waqāla mūsā yāfir'awnu innī rasūlum mir rabbil-'ālamīn
Na Musa alisema: Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 104
Maelezo ya chini
104 Musa akasema: Ewe Firauni! Hakika mimi nimetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote, Mwenye mamlaka juu ya mambo yao yote, ili nikufikishieni wito wake, na nikuiteni muifuate Sharia yake.