تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ ١٠١
Tilkal-qurā naqussu 'alayka min ambā'ihā walaqad jā'athum rusuluhum bil-bayyināti famā kānū liyu'minū bimā kaddhabū min qablu kadhālika yatba'ullāhu 'alā qulūbil-kāfirīn
Miji hiyo, tunakusimulia baadhi ya khabari zake. Na hapana shaka Mitume wao waliwafikia kwa hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini waliyo yakanusha zamani. Namna hivi Mwenyezi Mungu anazipiga muhuri nyoyo za makafiri. 101
Maelezo ya chini
101 Hiyo ni miji iliyo dumu karne nyingi, na imepitiwa na muda mrefu katika taarikhi yao. Tunakusimulia hivi sasa baadhi ya khabari zao zenye somo la kuzingatiwa. Na watu wa miji hiyo walifikiwa na Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi zenye kuonyesha ukweli wa wito wao. Lakini haikuwa shani yao kuamini baada ya kuja hizo Ishara zilizo wazi, kwa sababu ya mtindo wao wa kuwakanusha wasemao kweli. Basi wakawakadhibisha Mitume wao, wala hawakuongoka! Basi ni hivyo Mwenyezi Mungu huweka kizuizi juu ya nyoyo na akili za makafiri, ikafichika kwao Njia ya Haki, na wakajitenga nayo.