Surat Al-A'raf, aya 100

7:100

أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ ١٠٠

Awalam yahdi lilladhīna yarithūnal-arda mim ba'di ahlihā al law nashā'u asabnāhum bidhunūbihim wanatba'u 'alā qulūbihim fahum lā yasma'ūn

Je, hawahidiki hawa wanao rithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tutawapatiliza kwa madhambi yao, na tutapiga muhuri juu ya nyoyo zao, na kwa hivyo hawatasikia?. 100

Maelezo ya chini

100 Je, hawaujui mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa kaumu zilizo kwisha pita kabla yao, na kuwa shani yetu kwao ni kama ilivyo kuwa kwa walio watangulia? Na kwamba wao lazima wafuate tuyatakayo. Tukitaka kuwaadhibu kwa sababu ya madhambi yao tutawapatiliza kama tulivyo wapatiliza walio kama wao. Nasi tunatia muhuri nyoyo zao kwa kuwa zimeharibika bila ya kiasi, mpaka ikafika ukomo kuwa hazipokei tena uwongofu. Kwa muhuri huo imekuwa hawasikii hikima wala nasiha, kwa msikio wa kufahamu na kuwaidhika.