مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسۡرَىٰ حَتَّىٰ يُثۡخِنَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنۡيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ٦٧
Mā kāna linabiyyin an yakūna lahū asrā hattā yuthkhina fil-ardi turīdūna 'aradad-dunyā wallāhu yurīdul-ākhirata wallāhu 'azīzun hakīm
Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda baraabara katika nchi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima. 67
Maelezo ya chini
67 Haimfalii Nabii yeyote kukamata mateka, au kuchukua fidia, au kutoa bure msamaha, mpaka ashinde, na maadui waone wameshindwa, na wawe wamepata pigo kubwa hata kuwa hawawezi tena kupigana katika nchi. Lakini, nyinyi jamaa wa Kiislamu, mmefanya haraka katika Vita vya Badri kukamata mateka kabla hamjatamakani mkawa imara katika nchi. Mnatafuta manufaa ya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera, kwa kutukuzwa Neno la Haki, na lisikushughulisheni la dunia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda. Hukupangieni mambo yenu kwa mujibu wa faida yenu.