Surat Al-Anfal, aya 68

8:68

لَّوۡلَا كِتَٰبٞ مِّنَ ٱللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمۡ فِيمَآ أَخَذۡتُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ ٦٨

Llawlā kitābum minallāhi sabaqa lamassakum fīmā akhadhtum 'adhābun 'azīm

Lau isingeli kuwa hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingeli kupateni adhabu kubwa kwa vile mlivyo chukua. 68

Maelezo ya chini

68 Ingeli kuwa hapana hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumsamehe mwenye kujitahidi japo kuwa amekosa, basi ingeli kupateni adhabu kubwa kwa papara mliyo ifanya.