وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَٰرِهِم بَطَرٗا وَرِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ ٤٧
Walā takūnū kalladhīna kharajū min diyārihim bataran wari'ā'an-nāsi wayasuddūna 'an sabīlillāhi wallāhu bimā ya'malūna muhīt
Wala msiwe kama wale walio toka majumbani mwao kwa fakhari na kujionyesha kwa watu, na wakawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka yote wanayo yafanya. 47
Maelezo ya chini
47 Wala msiwe kama wale walio toka kwenye majumba yao, nao wana ghururi (udanganyifu) kwa nguvu na neema walizo nazo, wakijifakhari na kujionyesha mbele za watu, wakitaka wasifiwe kwa ushujaa na ushindi, na wao huku wanapinga watu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaupinga Uislamu. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitendo vyao kwa ujuzi na uwezo. Na Yeye atakuja walipa duniani na Akhera.