Surat Al-Anfal, aya 46

8:46

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُواْ فَتَفۡشَلُواْ وَتَذۡهَبَ رِيحُكُمۡۖ وَٱصۡبِرُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ ٤٦

Wa atī'ullāha warasūlahū walā tanāza'ū fatafshalū watadhhaba rīhukum wasbirū innallāha ma'as-sābirīn

Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. 46

Maelezo ya chini

46 Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika mambo mlio amrishwa na mlio katazwa. Na wacheni kuzozana na kukhitalifiana. Hayo ndiyo yanayo pelekea kupoteza nguvu na kushindwa. Na vumilieni mkipata shida za vita. Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanao vumilia wakasubiri kwa kuwapa msaada na kuwaunga mkono, na kuwalipa malipo mema.