Surat Al-Anfal, aya 48

8:48

وَإِذۡ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلۡيَوۡمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّي جَارٞ لَّكُمۡۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلۡفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكُمۡ إِنِّيٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوۡنَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ٤٨

Wa idh zayyana lahumush-shaytānu a'mālahum waqāla lā ghāliba lakumul-yawma minan-nāsi wa innī jārul lakum falammā tarā'atil-fi'atāni nakasa 'alā 'aqibayhi waqāla innī barī'um minkum innī arā mā lā tarawna innī akhāfullāha wallāhu shadīdul-'iqāb

Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. 48

Maelezo ya chini

48 Na kumbukeni, enyi Waislamu! Pale Shetani alipo kuja kuwazaini hawa washirikina kwa kuwaonyesha kuwa wayatendayo ni mazuri kwa uchochezi wake, akiwaambia: Hapana mtu ye yote anaye weza kuwashinda. Na akawahakikishia kuwa yeye atawalinda, na kuwanusuru! Yalipo kutana makundi mawili katika vita, vitimbi vyake na uchochezi wake ukavunjika. Akarejea nyuma, na akajitoa nao, akaogopa Mwenyezi Mungu asimuangamize. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.