Surat Al-An'am, aya 76

6:76

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبٗاۖ قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأٓفِلِينَ ٧٦

Falammā janna 'alayhil-laylu ra'ā kawkaban qāla hādhā rabbī falammā afala qāla lā uhibbul-āfilīn

Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipo tua akasema: Siwapendi wanao tua. 76

Maelezo ya chini

76 Ibrahim alimwomba Mola wake Mlezi, naye Mwenyezi Mungu akamhidi. Usiku ulipo kuja ukauziba mchana kwa kiza chake, akaona nyota inameremeta. Akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Ilipo potea, akasema kwa kuukataa ungu wa nyota: Sikubali kuabudu miungu inayo ondoka na kugeuka!