وَكَذَٰلِكَ نُرِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ مَلَكُوتَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلِيَكُونَ مِنَ ٱلۡمُوقِنِينَ ٧٥
Wakadhālika nurī ibrāhīma malakūtas-samāwāti wal-ardi waliyakūna minal-mūqinīn
Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini. 75
Maelezo ya chini
75 Kama alivyo ona Ibrahim - kwa tawfiqi yetu - upotovu wa watu wake katika kuyafanya masanamu ndio miungu, kadhaalika tumemwonyesha ufalme wetu mkubwa wa mbinguni na duniani na viliomo humo, ili aweze kusimamisha hoja kwa watu wake, na ili azidi kuamini.