Surat Al-An'am, aya 50

6:50

قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ٥٠

Qul lā aqūlu lakum 'indī khazā'inullāhi walā a'lamul-ghayba walā aqūlu lakum innī malakun in attabi'u illā mā yūhā ilayya qul hal yastawil-a'mā wal-basīru afalā tatafakkarūn

Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri? 50

Maelezo ya chini

50 Ewe Mtume! Waambie hawa makafiri: Mimi sikwambiini kuwa mimi nina madaraka aliyo nayo Mwenyezi Mungu hata nikuitikieni kwa mnayo yataka. Wala sidai kuwa mimi nina ilimu ya mambo ya ghaibu, ambayo Mwenyezi Mungu hakunijuvya. Wala sisemi kuwa mimi ni Malaika ninaweza kupanda mbinguni! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu tu. Sifuati ila Mwenyezi Mungu anacho nifunulia. Sema ewe Nabii: Je, wanakuwa sawa, aliye potoka na aliye ongoka katika kuzijua kweli hizi? Hivyo, inakuelekeeni nyinyi mkautupa uwongofu ninao kuleteeni, msiuzingatie kwa akili zenu hata ikakubainikieni Haki?