وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ ٥١
Wa andhir bihil-ladhīna yakhāfūna an yuhsharū ilā rabbihim laysa lahum min dūnihī waliyyun walā shafī'ul la'allahum yattaqūn
Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu. 51
Maelezo ya chini
51 Na wahadharishe kwa yaliyomo katika hii Qur'ani wale wanayo khofu vitisho vya Siku watapo wachunga Malaika kwa ajili ya hisabu na malipo, Siku ambayo itayo kuwa haina wa kunusuru wala kuombea ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wahadharishe wajitenge mbali na vinavyo mkasirisha Mwenyezi Mungu.