Surat Al-An'am, aya 44

6:44

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَبۡوَٰبَ كُلِّ شَيۡءٍ حَتَّىٰٓ إِذَا فَرِحُواْ بِمَآ أُوتُوٓاْ أَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ فَإِذَا هُم مُّبۡلِسُونَ ٤٤

Falammā nasū mā dhukkirū bihī fatahnā 'alayhim abwāba kulli shay'in hattā idhā farihū bimā ūtū akhadhnāhum baghtatan fa idhā hum mublisūn

Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuliwashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa. 44

Maelezo ya chini

44 Walipo acha kuwaidhika kwa ufakiri na maradhi tulio wapa kuwa ni mtihani, tukawajaribu baada yake kwa kuwapa riziki zenye wasaa. Tukawafungulia milango ya kila sababu za riziki, mpaka walipo furahia neema zetu, na wao wasimshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, ikawajia adhabu ghafla. Wakawa wanadahadari, wamekata tamaa, hawaipati njia ya kuokoka.