فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْۚ وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٥
Faquti'a dābirul-qawmil-ladhīna zalamū wal-hamdu lillāhi rabbil-'ālamīn
Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 45
Maelezo ya chini
45 Ikateketezwa kabisa kaumu hii, yenye kudhulumu, asibakie hata mmoja. Alhamdulillahi, wa kuhimidiwa kwa sifa zote njema ni Mwenyezi Mungu, mwenye kuwalea viumbe kwa neema na nakama, na mwenye kuisafisha ardhi na ufisadi wa wenye kudhulumu.