وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ ١٢١
Walā ta'kulū mimmā lam yudhkarismullāhi 'alayhi wa innahū lafisqun wa innash-shayātīna layūhūna ilā awliyā'ihim liyujādilūkum wa in ata'tumūhum innakum lamushrikūn
Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina. 121
Maelezo ya chini
121 Ilivyo kuwa hao wanyama ni halali kwenu kwa kuwachinja, basi msile yule ambaye hakutajiwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kumchinja, ikiwa limeachwa kutajwa makusudi, au limetajwa jina jingine lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani hivyo ni upotovu, na kutokana na hukumu ya Mwenyezi Mungu! Na hakika majeuri, Iblisi na wasaidizi wake, huwatia tia katika vifua vya wale walio kwisha watawala, ili wajadiliane nanyi kwa upotovu, na wakupelekeeni kuharimisha alivyo halalisha Mwenyezi Mungu. Nanyi mkiwafuata mtakuwa mfano wao katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu.