وَذَرُواْ ظَٰهِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَبَاطِنَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡسِبُونَ ٱلۡإِثۡمَ سَيُجۡزَوۡنَ بِمَا كَانُواْ يَقۡتَرِفُونَ ١٢٠
Wadharū zāhiral-ithmi wabātinahū innal-ladhīna yaksibūnal-ithma sayujzawna bimā kānū yaqtarifūn
Na acheni dhambi zilizo dhaahiri na zilizo fichikana. Hakika wanao chuma dhambi watalipwa kwa waliyo kuwa wakiyachuma. 120
Maelezo ya chini
120 Sio uchamngu kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu. Hakika uchamngu ni kuacha madhambi ya nje na ndani. Basi wacheni madhambi katika vitendo vyenu, vinavyo onekana na vilivyo fichika. Na bila ya shaka wanao chuma madhambi watalipwa kwa kadri ya madhambi wayatendayo.