فَلَوۡلَا نَصَرَهُمُ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ قُرۡبَانًا ءَالِهَةَۢۖ بَلۡ ضَلُّواْ عَنۡهُمۡۚ وَذَٰلِكَ إِفۡكُهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ٢٨
Falawlā nasarahumul-ladhīnat-takhadhū min dūnillāhi qurbānan ālihata bal dallū 'anhum wadhālika ifkuhum wamā kānū yaftarūn
Basi mbona wale walio washika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru? Bali waliwapotea! Na huo ndio uwongo walio kuwa wakiuzua. 28
Maelezo ya chini
28 Basi kwani hao walio wafanya miungu badala ya Mwenyezi Mungu ili iwakaribishe kwa Mwenyezi Mtukufu imeweza kuwakinga na maangamizo? Hasha! Bali miungu hiyo iliwakimbia, na hali wao ndio wana haja nayo mno iwanusuru. Na hayo yaliyo wafika, ya kutupwa na miungu yao, na kuwapotea ndio matokeo ya uwongo wao na uzushi wao.