Maswali ambayo watu huuliza

Somo la 7 kati ya 11

Kwa nini Waislamu hawali nguruwe wala hawanywi pombe?

Jibu kwa ufupi

Kwa sababu Allah ameviharamisha katika Kurani, na Waislamu wanamtii, wakiamini kwamba amri zake ni kwa faida yetu. Nyama ya nguruwe, damu, mzoga na nyama iliyochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allah ni haramu, ingawa mtu aliyelazimishwa na njaa bila njia nyingine hana lawama. Pombe na kila kilevi kingine pia ni haramu. Kurani inasema madhara yake ni makubwa kuliko faida yake, na kwamba huchochea chuki na kuwaweka watu mbali na Allah na swala.

Limeandikwa na Qabas na kuhakikiwa kwa kulinganishwa na Al-Mukhtasar fi Tafsir al-Qur'an al-Karim, Tafsir Ibn Kathir na maelezo ya HadeethEnc.com.

Kutoka Kurani

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ بِهِۦ لِغَيۡرِ ٱللَّهِۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Al-Baqarah 2:173Soma ndani ya Kurani

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ﴿٩٠﴾ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُوقِعَ بَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ فِي ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِ وَيَصُدَّكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَعَنِ ٱلصَّلَوٰةِۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?

Al-Ma'idah 5:90-91Soma ndani ya Kurani

۞ يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡخَمۡرِ وَٱلۡمَيۡسِرِۖ قُلۡ فِيهِمَآ إِثۡمٞ كَبِيرٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَإِثۡمُهُمَآ أَكۡبَرُ مِن نَّفۡعِهِمَاۗ وَيَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلِ ٱلۡعَفۡوَۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri--

Al-Baqarah 2:219Soma ndani ya Kurani

Kutoka Sunna

kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"

Imepokelewa na Muslim, vile vile Bukhari ikiwa na ibara ya mwisho ndani ya kitabu chake Sahihi HadeethEnc.com
Maelezo

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.

Masomo yote