Surat Yusuf, aya 75

12:75

قَالُواْ جَزَٰٓؤُهُۥ مَن وُجِدَ فِي رَحۡلِهِۦ فَهُوَ جَزَٰٓؤُهُۥۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ ٧٥

Qālū jazā'uhū man wujida fī rahlihī fahuwa jazā'uhū kadhālika najziz-zālimīn

Wakasema: Malipo yake ni yule ambaye ataonekana nalo yeye huyo ndiye malipo yake. Hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu. 75

Maelezo ya chini

75 Na kwa kuwa wana wa Yaa'qub walikuwa na yakini kuwa wao hawakukiba kile kikopo walisema bila ya kusitasita: Malipo ya mwenye kuchukua hicho kikopo ni kushikwa huyo na afanywe mtumwa. Ndio hivi sisi tunavyo walipa wenye kudhulumu wakachukua mali ya watu.