Surat Yusuf, aya 76

12:76

فَبَدَأَ بِأَوۡعِيَتِهِمۡ قَبۡلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسۡتَخۡرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِۚ كَذَٰلِكَ كِدۡنَا لِيُوسُفَۖ مَا كَانَ لِيَأۡخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ ٱلۡمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ وَفَوۡقَ كُلِّ ذِي عِلۡمٍ عَلِيمٞ ٧٦

Fabada'a bi aw'iyatihim qabla wi'ā'i akhīhi thummastakhrajahā min wi'ā'i akhīhi kadhālika kidnā liyūsufa mā kāna liya'khudha akhāhu fī dīnil-maliki illā an yashā'allāhu narfa'u darajātim man nashā'u wafawqa kulli dhī 'ilmin 'alīm

Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi. 76

Maelezo ya chini

76 Shauri ikaishia ipekuliwe mizigo, na ikawa lazima kufanya mambo baraabara ili isionekane kuwa kuna mpango ulio pangwa. Yusuf mwenyewe ndiye aliye fanya uchunguzi, baada ya kwisha tengeza mambo. Akaanza kupekua mizigo ya wale ndugu kumi, kisha ndio akaingia kuupekua mzigo wa nduguye. Humo akakitoa kile kikopo, na kwa hivyo hila yake ikafuzu. Akawa na haki kwa hukumu ya nduguze kumshika Bin-yamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyo mpangia mambo Yusuf. Hakuwa anaweza yeye kumshika nduguye kwa mujibu wa sharia ya mfalme wa Misri tu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Naye alitaka. Basi tulimpangia mambo Yusuf, na tukamwezesha kuzirekibisha sababu na mipango baraabara na hila nzuri. Na haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu, ambaye humtukuza katika vyeo vya ujuzi amtakaye. Na juu ya kila mwenye ilimu yupo mwenye kumzidia katika ujuzi!