Surat Yusuf, aya 63

12:63

فَلَمَّا رَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيهِمۡ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلۡكَيۡلُ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَآ أَخَانَا نَكۡتَلۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ ٦٣

Falammā raja'ū ilā abīhim qālū yā'abānā muni'a minnal-kaylu fa arsil ma'anā akhānā naktal wa innā lahū lahāfizūn

Basi walipo rejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi, basi mpeleke nasi ndugu yetu ili tupate kupimiwa; na yakini sisi tutamlinda. 63

Maelezo ya chini

63 Walipo rejea kwa baba yao walimsimulia kisa chao na Mheshimiwa wa Misri, na upole wake kwao, na kwamba amewaonya kuwa atawanyima kuwapimia chakula baadae ikiwa hatokuwa nao Bin-yamini; na kwamba amewaahidi kuwatimizia kipimo na atawatukuza pindi wakirudi na ndugu yao. Wakamwambia baba yao: Mwache ende nasi ndugu yetu, kwani ukimpeleka yeye tutapimiwa chakula cha kutosha tunacho kihitajia. Nasi tunakuahidi ahadi ya nguvu ya kwamba tutafanya juhudi kumlinda.