Surat Yusuf, aya 62

12:62

وَقَالَ لِفِتۡيَٰنِهِ ٱجۡعَلُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ فِي رِحَالِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَعۡرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ ٦٢

Waqāla lifityānihij'alū bidā'atahum fī rihālihim la'allahum ya'rifūnahā idhanqalabū ilā ahlihim la'allahum yarji'ūn

Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakapo rudi kwa watu wao wapate kurejea tena. 62

Maelezo ya chini

62 Walipo taka kuondoka aliwaambia wafwasi wake: Watilieni thamani ya bidhaa yao waliyo kuja nayo humo humo pamoja na mizigo yao, ili waione watakapo rudi kwa watu wao, wapate kurejea tena kwa kutumai kupewa chakula kwa kuamini kuwa tunatimiza ahadi, na wawe na imani ya usalama wa ndugu yao, na baba yao azidi kutua nafsi yake.