قَالَ هَلۡ ءَامَنُكُمۡ عَلَيۡهِ إِلَّا كَمَآ أَمِنتُكُمۡ عَلَىٰٓ أَخِيهِ مِن قَبۡلُ فَٱللَّهُ خَيۡرٌ حَٰفِظٗاۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ٦٤
Qāla hal āmanukum 'alayhi illā kamā amintukum 'alā akhīhi min qablu fallāhu khayrun hāfizan wahuwa arhamur-rāhimīn
Je, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote. 64
Maelezo ya chini
64 Yaa'qub yalimtibuka moyoni mwake yale ya zamani, akayaunganisha na haya mapya. Akawaambia wanawe: Nikikukubalieni itakuwa hali yangu ni ya ajabu; kwani nikikuaminini kwa huyu ndugu yenu haitakuwa ila mfano wa pale nilipo kuaminini kwa Yusuf. Mkamchukua kisha mkarudi mkisema: Kaliwa na mbwa mwitu! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye anaye nitosheleza katika kumlinda mwanangu. Wala mimi simtegemei mtu ila Yeye, kwani Yeye ndiye Mlinzi aliye na nguvu kuliko wote, na rehema yake ni kunjufu mno, hatonipa tena machungu ya ndugu yake baada ya yale ya Yusuf.