Surat Yunus, aya 65

10:65

وَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًاۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٦٥

Walā yahzunka qawluhum innal-'izzata lillāhi jamī'an huwas-samī'ul-'alīm

Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. 65

Maelezo ya chini

65 Ewe Mtume! Usihuzunuke kwa wayasemayo washirikina ya kejeli, na matusi, na kukadhibisha. Wala usidhani kuwa hali yao hii itadumu. Bali ushindi ni wako, na Uislamu utatukuka, kwani utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ushindi upo mkononi mwake, na Yeye atakunusuru uwashinde hao makafiri. Na Yeye Subhanahu ni Mwenye kuyasikia wanayo kuzulia, na Mwenye kuyajua wanayo dhamiria. Na Yeye atawalipa kwa hayo.