أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا يَتَّبِعُ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُرَكَآءَۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ ٦٦
Alā inna lillāhi man fis-samāwāti waman fil-ardi wamā yattabi'ul-ladhīna yad'ūna min dūnillāhi shurakā'a in yattabi'ūna illaz-zanna wa in hum illā yakhrusūn
Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na ardhinii.Na wala hawawafuati hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake. Wao hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo. 66
Maelezo ya chini
66 Enyi watu! Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu peke yake vyote viliomo mbinguni na duniani, kwa kuviumba, na kuvimiliki, na kuviendesha. Na hao wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu kwa hakika hawawafuati hao miungu ya ushirikina. Hao si chochote ila wanafuata mawazo tu, wanadhani kuwa uwezo umo katika vitu ambavyo havijifai wenyewe, la kwa manufaa wala madhara.