Surat Yunus, aya 64

10:64

لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ٦٤

Lahumul-bushrā fil-hayawātid-dunyā wafil-ākhirati lā tabdīla likalimātillāhi dhālika huwal-fawzul-'azīm

Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 64

Maelezo ya chini

64 Kwa wapenzi hawa wa Mwenyezi Mungu pana bishara ya kheri hapa duniani, kwa vile Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwapa ushindi na utukufu, na Akhera itatimia ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu haigeuki. Na haya ndiyo waliyo bashiriwa kwayo duniani, na watayapata Akhera. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.