وَمِنۡهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تَهۡدِي ٱلۡعُمۡيَ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يُبۡصِرُونَ ٤٣
Waminhum man yanzuru ilayka afa'anta tahdil-'umya walaw kānū lā yubsirūn
Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni? 43
Maelezo ya chini
43 Na wengine wapo wanao kutazama na wanalifikiria jambo lako, na wanaona dalili zilizo wazi za Unabii wako. Lakini bado hawaongoki wakafuata. Mfano wa hayo ni mfano wa kipofu, nawe huwezi kuwaongoa hao vipofu. Upofu wa macho ni kama upofu wa moyo. Wote hawana uwongofu! Kipofu haioni njia kwa kuhisi, na mpotovu haongoki kwa maana.