Surat Yunus, aya 42

10:42

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يَعۡقِلُونَ ٤٢

Waminhum man yastami'ūna ilayka afa'anta tusmi'us-summa walaw kānū lā ya'qilūn

Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza. Je, wewe unaweza kuwafanya viziwi wasikie ijapo kuwa hawafahamu? 42

Maelezo ya chini

42 Na katika hawa makafiri wapo wanao kusikiliza wewe, Mtume, pale unapo waita wafuate Dini ya Mwenyezi Mungu, na hali nyoyo zao zimefungwa hazikubali Wito wako. Basi wewe huwezi kuwafanya hawa viziwi wakusikie na waongoke. Na khasa ilivyo kuwa juu ya uziwi wao, hawafahamu uyasemayo.