Surat Yunus, aya 44

10:44

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ ٱلنَّاسَ شَيۡـٔٗا وَلَٰكِنَّ ٱلنَّاسَ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ٤٤

Innallāha lā yazlimun-nāsa shay'an walākinnan-nāsa anfusahum yazlimūn

Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao. 44

Maelezo ya chini

44 Hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu atawalipa watu kwa vitendo vyao kwa uadilifu na haki, wala hatamdhulumu hata mmoja wapo kwa kitu chochote. Lakini watu wanajidhulumu nafsi zao kwa kukhiari kwao ukafiri kuliko Imani.