Surat Yunus, aya 39

10:39

بَلۡ كَذَّبُواْ بِمَا لَمۡ يُحِيطُواْ بِعِلۡمِهِۦ وَلَمَّا يَأۡتِهِمۡ تَأۡوِيلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ ٣٩

Bal kaddhabū bimā lam yuhītū bi'ilmihī walammā ya'tihim ta'wīluhū kadhālika kaddhabal-ladhīna min qablihim fanzur kayfa kāna 'āqibatuz-zālimīn

Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhaalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa mwisho wa madhaalimu hao. 39

Maelezo ya chini

39 Bali hawa washirikina wamekimbilia kuikadhibisha Qur'ani bila ya kuzingatia, wakajua yaliomo ndani yake! Wao wenyewe hawakutazama mna nini, wala hawakusita kuitafuta tafsiri yake, na kutaka kuelewa hukumu zake kwa kuwauliza wenginewe! Na kukadhibisha namna hii bila ya ujuzi, ndivyo walivyo wakanusha makafiri wa kaumu za zamani Mitume wao na Vitabu vyao! Basi, ewe mwanaadamu! Angalia yaliishiaje mambo ya walio kadhibisha walio tangulia. Waliachiliwa mbali na wakateketezwa kwa adhabu! Na huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa mfano wa hao.