أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٣٨
Am yaqūlūnaftarāhu qul fa tū bisūratim mithlihī wad'ū manistata'tum min dūnillāhi in kuntum sādiqīn
Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. 38
Maelezo ya chini
38 Bali hawa washirikina wanasema: Muhammad kaizua hii Qur'ani mwenyewe! Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hii Qur'ani ni kazi ya mwanaadamu, basi nyinyi leteni Sura moja tu mfano wake, na muwatake muwatakao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, waje kukusaidieni; ikiwa nyinyi ni wasema kweli katika madai yenu kuwa hii Qur'ani nimeitunga mimi.