وَمِنۡهُم مَّن يُؤۡمِنُ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن لَّا يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ ٤٠
Waminhum man yu'minu bihī waminhum mal lā yu'minu bihī warabbuka a'lamu bil-mufsidīn
Na miongoni mwao wapo wanao iamini, na miongoni mwao wapo wasio iamini. Na Mola wako Mlezi anawajua vyema mafisadi. 40
Maelezo ya chini
40 Na miongoni mwa hawa wakanushao wapo ambao watakuja iamini Qur'ani baada ya kuyafahamu yaliyomo ndani yake, na wakayaelewa maana yake. Na kipo miongoni mwao kikundi ambacho hakiamini wala hakiachi upotovu wake! Na Allah Subhanahu wa Taa'la anawajua vyema wakanushao mafisadi, na atawalipa kwa vitendo vyao.