وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تُؤۡمِنَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَجۡعَلُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ ١٠٠
Wamā kāna linafsin an tu'mina illā bi idhnillāhi wayaj'alur-rijsa 'alal-ladhīna lā ya'qilūn
Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao. 100
Maelezo ya chini
100 Hawezi mtu kuamini ila akiielekeza nafsi yake kwa hayo, na Mwenyezi Mungu akamsahilishia sababu na njia za hayo. Ama yule asiye ielekea Imani huyo basi amestahiki kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu, na kupata adhabu yake. Na mwendo wa Mwenyezi Mungu ni kuwapa adhabu na ghadhabu wale wanao zipuuza na kuzikataa hoja zilio wazi, na wala hawazizingatii.