وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَأٓمَنَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ كُلُّهُمۡ جَمِيعًاۚ أَفَأَنتَ تُكۡرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ ٩٩
Walaw shā'a rabbuka la'āmana man fil-ardi kulluhum jamī'an afa'anta tukrihun-nāsa hattā yakūnū mu'minīn
Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini? 99
Maelezo ya chini
99 Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka watu wote katika ardhi waamini, wangeli amini. Basi wewe usihuzunike kwa ukafiri wa washirikina. Wala haiwi Imani ila kwa khiari. Basi wewe huwezi kuwalazimisha watu kwa nguvu ili wafuate Haki na waitikie. Haikupasii kutaka kuwalazimisha waamini, wala hutoweza, hata ukijitahidi vipi.