وَلَهُمۡ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَمَشَارِبُۚ أَفَلَا يَشۡكُرُونَ ٧٣
Walahum fīhā manāfi'u wamashāribu afalā yashkurūn
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? 73
Maelezo ya chini
73 Na wanapata kwa hao vitu vya kuwapa manufaa, kama sufi, na manyoya, na nywele, na ngozi, na mafupa, na vinywaji kutokana na maziwa yao. Je! Wanasahau neema hizi hata wamekuwa hawamshukuru aliye waneemesha?