Surat Yasin, aya 36

36:36

سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡأَزۡوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلۡأَرۡضُ وَمِنۡ أَنفُسِهِمۡ وَمِمَّا لَا يَعۡلَمُونَ ٣٦

Subhānal-ladhī khalaqal-azwāja kullahā mimmā tumbitul-ardu wamin anfusihim wamimmā lā ya'lamūn

Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. 36

Maelezo ya chini

36 Wa kutakasika ni Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu kwa mpango wa ume na uke, katika mimea na katika nafsi zao watu, na katika vitu ambavyo watu hawavijui. Hii harufi Min , yaani "Katika" katika Aya hii ni ya kubainisha. Maana yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba madume na majike katika viumbe vyake vyote, sawa sawa katika mimea, na wanyama, na wanaadamu na vyenginevyo ambavyo watu hawavijui na hawavioni.