Surat Yasin, aya 37

36:37

وَءَايَةٞ لَّهُمُ ٱلَّيۡلُ نَسۡلَخُ مِنۡهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظۡلِمُونَ ٣٧

Wa āyatul lahumul-laylu naslakhu minhun-nahāra fa idhā hum muzlimūn

Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. 37

Maelezo ya chini

37 Na Ishara pia ya kuwepo Mwenyezi Mungu na uweza wake, ni huu usiku ambao tunautoa ndani yake mchana, kama kuivua nguo inayo sitiri. Mara utaona watu wamo gizani lilio wazunguka kila upande.