Surat Sad, aya 19

38:19

وَٱلطَّيۡرَ مَحۡشُورَةٗۖ كُلّٞ لَّهُۥٓ أَوَّابٞ ١٩

Wat-tayra mahshūratan kullul lahū awwāb

Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake. 19

Maelezo ya chini

19 Na pia tukamdhalilishia ndege walio kusanywa kutokana na kila namna na kila pahali. Vyote hivyo, milima na ndege, vikimwitikia Daudi kama atakavyo, akivisarifu kama apendavyo kwa maslaha ya umma.