Rabbij'alni muqimas-salah

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

رَبِّ ٱجۡعَلۡنِي مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِيۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلۡ دُعَآءِ ٤٠

Rabbij'alnī muqīmas-salawāti wamin dhurriyyatī rabbanā wataqabbal du'ā'

Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Swala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. 40

Maelezo ya chini

40 Ewe Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nitimize Swala kwa inavyo takikana. Na wawezeshe watimilize kadhaalika wale walio wa kheri katika dhuriya zangu. Ewe Mola wetu Mlezi ipokee dua yangu kwa mapokezi ya kukubaliwa.

رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ يَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡحِسَابُ ٤١

Rabbanaghfir lī waliwālidayya walil-mu'minīna yawma yaqūmul-hisāb

Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. 41

Maelezo ya chini

41 Ewe Mola wetu Mlezi! Nisamehe madhambi yaliyo niponyoka, na wasamehe wazazi wangu, na Waumini wote, Siku itapo hakikishwa hisabu, na baadae ikawa malipo.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Ibrahim yote

Maswali

Rabbij'alni muqimas-salah iko wapi katika Qur'ani?

Rabbij'alni muqimas-salah iko katika Surat Ibrahim, 14:40-41.