Surat Ibrahim, aya 40

14:40

رَبِّ ٱجۡعَلۡنِي مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِيۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلۡ دُعَآءِ ٤٠

Rabbij'alnī muqīmas-salawāti wamin dhurriyyatī rabbanā wataqabbal du'ā'

Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kushika Swala, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu Mlezi, na ipokee dua yangu. 40

Maelezo ya chini

40 Ewe Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nitimize Swala kwa inavyo takikana. Na wawezeshe watimilize kadhaalika wale walio wa kheri katika dhuriya zangu. Ewe Mola wetu Mlezi ipokee dua yangu kwa mapokezi ya kukubaliwa.