وَلَوۡ أَنَّمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن شَجَرَةٍ أَقۡلَٰمٞ وَٱلۡبَحۡرُ يَمُدُّهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦ سَبۡعَةُ أَبۡحُرٖ مَّا نَفِدَتۡ كَلِمَٰتُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ٢٧
Walaw annamā fil-ardi min shajaratin aqlāmun wal-bahru yamudduhū mim ba'dihī sab'atu abhurim mā nafidat kalimātullāhi innallāha 'azīzun hakīm
Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingeli kwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. 27
Maelezo ya chini
27 Na lau kuwa miti yote ya duniani ikageuka kalamu, na maji yote ya baharini kwa wingi wake yakageuka wino, kuandikia maneno ya Mwenyezi Mungu, basi zingeli kwisha kalamu na wino ukamalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mwenyezi Mungu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, hashindwi na chochote, Mwenye hikima hakimfutu kitu katika ujuzi wake na hikima yake. Basi hayeshi maneno yake na hikima yake.