مَّا خَلۡقُكُمۡ وَلَا بَعۡثُكُمۡ إِلَّا كَنَفۡسٖ وَٰحِدَةٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ ٢٨
Mmā khalqukum walā ba'thukum illā kanafsin wāhidatin innallāha samī'u basīr
Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. 28
Maelezo ya chini
28 Kukuumbeni nyinyi hapo mwanzo na kukufufueni baada ya kufa, mbele ya uweza wa Mwenyezi Mungu si chochote ila ni kama kumuumba na kumfufua mtu mmoja tu. Hakika Mwenyezi Mungu anaisikia kauli ya washirikina wanapo sema ati: Hakuna kufufuliwa. Naye ni Mwenye kuviona vitendo vyao, naye atawalipa kwavyo.