Surat Hud, aya 77

11:77

وَلَمَّا جَآءَتۡ رُسُلُنَا لُوطٗا سِيٓءَ بِهِمۡ وَضَاقَ بِهِمۡ ذَرۡعٗا وَقَالَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَصِيبٞ ٧٧

Walammā jā'at rusulunā lūtan sī'a bihim wadāqa bihim dhar'an waqāla hādhā yawmun 'asīb

Na wajumbe wetu walipo kuja kwa Lut' aliwahuzunukia na akawaonea dhiki. Akasema: Hii leo ni siku ngumu! 77

Maelezo ya chini

77 Walipo kuja wajumbe wetu, hao Malaika, kwa Lut' kwa sura ya vijana wazuri, Lut' aliungulika na akaudhika. Alihisi unyonge hana nguvu za kuwahami na hao watu wake, akawaonea dhiki kwa kuwaogopea ufisadi wa kaumu yake! Akasema: Hii leo ni siku ya karaha kubwa na machungu!