Surat Hud, aya 76

11:76

يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ أَعۡرِضۡ عَنۡ هَٰذَآۖ إِنَّهُۥ قَدۡ جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَإِنَّهُمۡ ءَاتِيهِمۡ عَذَابٌ غَيۡرُ مَرۡدُودٖ ٧٦

Yā'ibrāhīmu a'rid 'an hādhā innahū qad jā'a amru rabbika wa innahum ātīhim 'adhābun ghayru mardūd

(Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Kwa hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyo rudi nyuma. 76

Maelezo ya chini

76 Malaika wakasema: Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya majadiliano, na kuwatakia rehema watu hawa. Kwani amri ya Mola wako Mlezi ya kuwaangamiza imekwisha kuja! Hapana budi kuwa adhabu itawashukia, na wala haitarudishwa kwa majadiliano au bila ya majadiliano.