وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ ٧٨
Wajā'ahū qawmuhū yuhra'ūna ilayhi wamin qablu kānū ya'malūnas-sayyi'āti qāla yāqawmi hā'ulā'i banātī hunna atharu lakum fattaqullāha walā tukhzūni fī dayfī alaysa minkum rajulur rashīd
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka? 78
Maelezo ya chini
78 Watu wake wakajua kuwa wamekuja wale wageni, wakamwendea mbio mbio. Na kabla ya hayo ilikuwa kazi yao kufanya huo uchafu wao na kutenda maovu! Lut' akawaambia: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, waoeni. Hao ni safi zaidi kwenu kuliko kwenda kufanya uchafu kwa wanaume! Mwogopeni Mwenyezi Mungu, na jilindeni nafsi zenu na adhabu yake; na msinifedhehi na mkanidharaulisha kwa kuwavamia wageni wangu! Basi hivyo hamna kati yenu hata mtu mmoja mwenye rai iliyo sawa, mwenye akili iliyo ongoka, akakuzuieni na maasi na akakukatazeni maovu?