وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ ٧١
Wamra'atuhū qā'imatun fadahikat fabassharnāhā bi ishāqa wamin warā'i ishāqa ya'qūb
Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub. 71
Maelezo ya chini
71 Na mkewe alikuwa kasimama karibu akisikia maneno yao. Akacheka kwa furaha ya kuwa mwenyewe Lut', ambaye ni mtoto wa ndugu wa mumewe, atasalimika. Basi Sisi tulimbashiria kwa ndimi za wale Malaika kuwa atamzalia mumewe Ibrahimu mtoto mwanamume ataye itwa Is-haq, na huyo mtoto ataishi, na baadae Is-haq atampata Yaaqub.